MLAJI 1;Enyi walaji wa leyo, kusema nanyi nataka Ipunguzeni pupiyo, lasivyo mtadhurika Nyoyo zipeni zuiyo, mwili utabusarika Shikilia wako moyo, mlaji utaumia. 2;Mnapopita shambani, matunda yawazuzuwa Mboga hamzitamani, zawachosha kuchambuwa Macho yote yamtini, paku mnaupekuwa Shikilia wako moyo, mlaji utaumia. 3;Muonapo tunda pera, limelala kidarini Nyanyachungu ama tura, mbili mbili zi tawini Kwa kebehi mnafura, mwasema hizi za nini Shikilia wako moyo, mlaji utaumia. 4;Mwataka ulojazia, mti hadi mashinani Ili ukiupandia, uhisi u kitandani Huku dodo wajilia, wajipea burudani Shikilia wako moyo, mlaji utaumia. 5;Muonapo ni papai, au dodo mwalichuma Mwajitia ubedui, kulipapasa kwa nyuma Kifuatacho jimai, kichwani mwawaza nyama Shikilia wako moyo, mlaji utaumia. 6;Kisha hufata vurugu, za kwichi kwichi mtini Yale mavuno ya njugu, mli...
Karibu kwenye ukurasa wa mashairi ya mwambao, mahali pekee unapoweza kupata mashairi ya lugha ya kiswahili, yenye kuituliza na kuikonga nafsi yako. Karibu na ahsante kwa kujumuika nasi!.