BWANA DHIKI 1;Hana baba wala mama,wala ndugu wa kunusa Halali ndani ya hema,jua mvua yamtosa Ngozi yake ya ukoma,ngumu kwa kuipapasa Wamuita bwana dhiki,jinale yake maisha. 2;Hana kazi wala bazi,anafanya dei waka Elimu hana ujuzi,darasani hakufika Machinga na wachuuzi,humfanya kibaraka Wamuita bwana dhiki,jinale yake maisha. 3;Kuu kuu nguo zake,mabwende yalotoboka Waume kwa wanawake,husema amechizika Upitapo kando yake,uvundo unamnuka Wamuita bwana dhiki,jinale yake maisha. 4;Sura yake ni nyeusi,tii yenye kupauka Mfupi kama kipisi,ama shina la mugoka Mapele kama fenesi,ngoziye imebabuka Wamuita bwana dhiki,jinale yake maisha. 5;Watupavyo jalalani,vyote vilo haribika Ndizi mboga za majani,na nyama zinazo nuka Hushindilia tumboni,haogopi kudhurika Wamuita bwana dhiki,jinale yake maisha. 6;Yupo peku miguuni,kokoto zinamng'ata Apitapo jalalani,vigae v...
Mashairi ya mwambao
Karibu kwenye ukurasa wa mashairi ya mwambao, mahali pekee unapoweza kupata mashairi ya lugha ya kiswahili, yenye kuituliza na kuikonga nafsi yako. Karibu na ahsante kwa kujumuika nasi!.